Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-GBAGBO-NGESSAN-FPI-UCHAGUZI-SIASA

Côte d’Ivoire: FPI yatangaza wagombea 2 kwenye uenyekiti wa chama

Chama cha rais wa zamani wa Côte d’Ivoire Laurent Gbagbo, ambaye sasa anashikiliwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kimemweka Gbagbo katika orodha ya wagombea uenyekiti wa chama hicho cha FPI na kutangaza maombi yake kuwa halali.

Laurent Gbagbo, mwenyekiti wa zamanai na mwasisi wa chama cha FPI (kushoto) na Pascal Affi N'Guessan, mwenyekiti wa FPI anaye maliza muda wake (kulia).
Laurent Gbagbo, mwenyekiti wa zamanai na mwasisi wa chama cha FPI (kushoto) na Pascal Affi N'Guessan, mwenyekiti wa FPI anaye maliza muda wake (kulia). Reuters
Matangazo ya kibiashara

Baada ya wiki kadhaa ya mvutano na mgogoro wa ndani ya chama, hatimaye watu wawili akiwemo Gbagbo mwenyewe ndio watakaogombea kinyanganyiro hicho mjini Abidjan, mpinzani wake akiwa waziri mkuu wa zamani Pascal Afy Ngessan.

Kamati ya ukaguzi ilikuwa ikitathmini iwapo faili za wagombea wote wawili zinatimiza masharti pamoja na kasoro ziliyotajwa na kila mmoja dhidi ya mwengine.

Kwa hiyo kamati hiyoiliamua bila kupendelea upande wowote kupasisha majina ya watu hao wawili kugombea kwenye uenyekititi wa chama cha FPI, ambacho kwa sasa kinaonekana chama kikuu cha upinzani nchini Côte d’Ivoire.

Ni kwenye makao makuu ya chama cha FPi ambapo kulifanyika mkutano wa kutathmini faili za watu hao pamoja na kujadili namna ya kutafutia suluhu mvutano uliokua umejitikeza kuhusu nani atayekua mwenyekiti wa chama.

Msemaji wa kamati hiyo, Gniapa Godé amesema uteuzi Laurent Gbagbo ni halali kwa kuwa mwenyekiti wa chama alichoanzisha mwaka 1982. Taarifa ambayo aliitoa mbele ya wafuasi na wajumbe wa chama hicho kilichokua kikiongozwa na aliye kua rais wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.