Pata taarifa kuu

Uchaguza Tunisia: uwezekano wa kuingia duru ya pili

Nchini Tunisia, inaelekea wagombea wakuu wawili wanaonwania urais nchini humo watapambana katika duru ya pili ya kumchagua rais tarehe 31 mwezi ujao wa Desemba.

idadi ya wapiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais Tunisia ilikuwa ndogo kuliko uchaguzi wa wabunge.
idadi ya wapiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais Tunisia ilikuwa ndogo kuliko uchaguzi wa wabunge.
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa mkongwe Beji Caid Essebsi, ambaye chama chake kilipata ushindi mkubwa wakati wa uchaguzi wa wabunge mwezi uliopita inaoneka atashindwa kupata ushindi wa asilimia 50 unaohitajika ili kuwa mshindi wa moja kwa moja.

Essebsi atapambana na rais wa sasa Moncef Marzouki, ambaye amekuwa akiiongoza nchi hiyo tangu kutokea kwa mapinduzi nchini humi mwaka 2011.

Jumuiya ya Kimataifa ikiongozwa na Marekani imepongeza Tunisia kuonesha mfano mzuri wa ukuaji wa Demokrasia kwa kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwishoni mwa juma lililopita ulifanyika kwa njia ya amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.