Pata taarifa kuu
NIGERIA-APC-BOKO HARAM-Siasa-Usalama

Nigeria: Chama cha upinzani cha APC chaituhumu polisi

Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria APC kimewatuhumu maafisa wakuu wa usalama nchini humo kwa kuendesha uporaji kwenye ofisi zao katika mji mkuu wa Lagos. 

Raia wa Nigeria wakifuatilia magazeti kuhusu uchaguzi mkuu
Raia wa Nigeria wakifuatilia magazeti kuhusu uchaguzi mkuu REUTERS/Temilade Adelaja
Matangazo ya kibiashara

Hali hiyo imetokea wakati ambapo nchi hiyo ikijiandaa kuelekea kwenye uchaguzi mwezi february mwakani.

Chama hicho kimebaini kwamba polisi imewakamata baadhi ya wafanyakazi kwenye ofisi hizo.

Chama hicho cha upinzani kinadai wafanya kazi wake ishirini na nane walikamatwa na polisi siku ya jumamosi na kwamba hadi kufika sasa hawajuwi sababu zozote za kukamatwa kwao.

Hali hiyo imetokea wakati mashirika mbalimbali ya kimataifa yamekua yakitahadhari kutokea kwa machafuko kutokana na mvutano wa kisiasa unaoendelea

Hayo yanajiri huku kukiwa na taarifa kwamba Waasi wa kundi la Boko Haram nchini humo iliwaua wafanyabiashara 48 wa kuuza samaki katika jimbo la Borno karibu na mpaka na nchi jirani ya Chad wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.