Pata taarifa kuu
MISRI-ULAYA-H5N1-H5N8-Afya

Misri: homa ya ndege yaua watu wawili, Ulaya yatiwa wasiwasi

Virusi H5N1 vimewaua watu wawili ndani ya siku mbili nchini Misri. Wakati huohuo baadhi ya mifugo imeshambuliwa na aina nyingine ya virusi barani Ulaya, hususan kaskazini mashariki mwa Ujerumani, Uholanzi na Uingereza, kwa mujibu wa shirika la afya ya wanyama duniani.

Virusi H5N8 vinavyosababisha aina nyingine ya Homa ya ndege, ambavyo ni hatari kwa mwanadamu, vyagunduliwa Ulaya, Novemba 17 mwaka 2014.
Virusi H5N8 vinavyosababisha aina nyingine ya Homa ya ndege, ambavyo ni hatari kwa mwanadamu, vyagunduliwa Ulaya, Novemba 17 mwaka 2014. France 24
Matangazo ya kibiashara

Mtu wa pili kubainika kuwa na virusi H5N1 vinavyosababisha homa ya ndege alifariki Jumanne Novemba 18 nchini Misri na kutimiza idadi ya watu watatu kufariki kutokana na homa hiyo mwaka huu nchini humo, shirika la habari la Al-Haram limechapisha kwenye mtandao wake.

Mtu huyo aliyefariki kutokana na Homa ya ndege ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30, mkaazi wa mkoa wa Minya, kusini mwa Cairo, limeongeza shirika hilo, likinukuu taarifa iliyotolewa na wizara ya afya.

Jumatano Novemba 17, msichana mwenye umri wa miaka 19 alifariki baada ya kusogelea ndege walioambukizwa. Msichana huyo alifariki katika hospitali ya mji wa Assiout, katikati mwa nchi.

Virusi H5N1 vinavyosababisha Homa ya ndege vimewaua watu 400 hasa kusini mashariki mwa Asia tangu vilipogunduliwa.

Katika bara kongwe la Ulaya, visa vya Homa ya ndege H5N8 viliorodheshwa nchini Ujerumani, mwanzoni mwa mwezi Novemba, na baadae Uholanzi na kisha kaskazini mwa Uingereza Jumanne Novemba 18 mwaka 2014.

Virusi H5N8 mpaka sasa vimeonekana katika bara la Asia, laikini mara ya kwanza viligunduliwa Uholanzi, ambapo ndege 150,000 ikiwa ni pamoja na kuku na bata waliuawa.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa magonjwa ya mambukizi kwenye Shirika la Afya duniani (WHO), Elizabeth Mumford, visa vingine vya virusi H5N8 huenda vikagunduliwa kwa wanyama pori.

Elizabeth Mumford, amewatolea wito viongozi mbalimbali kua makini dhidi ya virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.