Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-JESHI-MAANDAMANO-USALAMA

Cote d'Ivoire: "rais ameelewa" malalamiko ya wanajeshi

Wanajeshi kutoka maeneo mbalimbali nchini Cote d'Ivoire waliandamana Jumanne Novemba 18 wakidai malipo ya malimbikizo ya mishahara yao, ambayo kwa baadhi inadumu miaka mingi.

Wanajeshi wa Cote d'Ivoire wakizuia barabara zinazoingia katika eneo la kibiashara la Plateau, Abidjan, Novemba 18 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Cote d'Ivoire wakizuia barabara zinazoingia katika eneo la kibiashara la Plateau, Abidjan, Novemba 18 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Maandamano hayo yalisambaa nchini nzima, hususan, Bouaké, Abidjan, Ferkéssédougou, Korhogo, Bondoukou pamoja na Abengourou.

Katika mji wa Bouaké, wanajeshi walikiteka kwa muda wa saa moja na nusu kituo cha redio na televisheni cha taifa RTI.
Katika mji wa Abobo, wanajeshi wamesema kwamba wamevumilia kipindi kirefu , kwa hiyo wameamua kuendelea na maandamano hadi pale madai yao yatapatiwa ufumbuzi

“ Tangu mkataba wa Ouagadougou, tulisubiri, kwa sababbu tulifahamu kwamba nchi inakabiliwa na wakati mgumu. Kati ya Januari 1 mwaka 2009 hadi mwezi Juni mwaka 2011, hakuna mshahara tuliyopewa”. Rais anatakiwa kuchukua hatua ili kupatia suluhu hali hii. Anapaswa kusema “ madai yenu yamepatiwa ufumbu”, " kauli hiyo ndio tunataka kusikia”, amesema mwanajeshi mmoja.

Serikali ya Cote d'Ivoire imeahidi kushughulikia madai hayo na kuwataka wanajeshi wa nchini humo kuwa watulivu kama alivyobainisha.

“ Ninachotaka kuwambia vijana. Kwa kweli mumejieleza na malalamiko yenu rais ameyazingatia. Rais ameliomba Bunge kujadili madai yenu yaweze kupatiwa ufumbuzi”, amesema Waziri wa mambo ya ndani, Ahmed Bakayoko

Awali Waziri wa Ulinzi Paul Koffi Koffi alitangaza kuchukua baadhi ya hatua, huku akiahidi kuwa wanajeshi hao watapewa mishahara yao hivi karibuni.

" Nusu ya malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi wa zamani 476 wa FDS itatolewa mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2014 na nusu nyingine itatolewa mwisho wa mwezi Desemba mwaka 2014", alisema Waziri wa Ulinzi Paul Koffi Koffi.

Imearifiwa kuwa hali ya utulivu imerejea katika baadhi ya miji nchini Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.