Burundi: Tume ya uchaguzi yaendelea kunyooshea kidole
Wajumbe wa tume ya uchaguzi kwenye ngazi za wilaya nchini Burundi wanatazamiwa kula kiapo Jumatano Novemba 5, huku chama cha NFL kikisema bado hakijapata jibu kuhusu kasoro zilizoibuka kuhusu uteuzi wa wajumbe hao, kwa maandalizi ya Uchaguzi wa mwaka wa 2016.
Imechapishwa:
Cheza - 05:05
Muungano wa vyama vya upinzani ADC-Ikibri pamoja na baadhi ya mashirika ya kiraia viliamua hivi karibuni kuwaondoa wajumbe wao katika tume hiyo.
Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi nchini Burundi Ceni, imekua ikinyooshewa kidole na vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia pamoja na vyama vinavyounga mkono utawala wa chama tawala Cndd-fdd kwa kuchukua uamzi bila kuwashirikisha wadau wote katika suala la uchaguzi.
Tume hiyo ilipingwa na vyama vya upinzani tangu ilipoteuliwa na kupasishwa na Bunge mwanzoni mwa mwaka 2014. Hata hivo tume hiyo Ceni ilituhumiwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwamba ilipanga njama na chama tawala Cndd-Fdd kwa kuiba kura, ziliyopelekea ushindi wa chama cha Cndd-Fdd.