Pata taarifa kuu
DRC-Sheria

DRC : Padiri Appolinaire Malu Malu ahojiwa mahakamani

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), Padiri Appolinaire Malu Malu amehojiwa kwa muda wa saa kadhaa katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu jumatatu wiki hii mjini Kinshasa kwa uchunguzi wa awali.

Padiri bAppolinaire Malu Malu, ambaye anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma
Padiri bAppolinaire Malu Malu, ambaye anakabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa mali ya umma (Photo : AFP)
Matangazo ya kibiashara

Padri Malu Malu amefunguliwa mashtaka kwenye mahakama kuu nchini humo kufuatia malalamiko ya vyama vya upinzani chini ya sheria ya mwaka 2010 ya makosa katika manunuzi kwa sekta ya umma , kashfa iliyoibuliwa na kufikishwa mahakamani na wapinzani wasiopungua mia moja.

Kulingana na vyanzo vya karibu na Mwendesha Mashtaka Mkuu huyo utaratibu huo atakaokabiliana na Padri Malu Malu utalilazimu Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kumuondolea Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kinga ya cheo chake hatua ambayo Mahakama inatarajiwa kuifikia hivi karibuni.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuwachia kiongozi huyo, Delion Kimbulungu ambaye ni mshauri wa mawasiliano wa Malu Malu, amesema kuwa Padiri huyo amealikwa kwa mazungumzo yanayotokana na mwaliko rasmi ili kupitia masuala ya kisheria yatokanayo na uchaguzi na si vinginevyo kama ilivyotangazwa na vyombo vya habari nchini DRC.

Hata hivyo, vyanzo vya mahakama, ambavyo havikupendelea majina yao yatajwe, vimebaini kuwa Padiri Appolinaire Malu Malu ameitishwa na Mahakama kwa uchunguzi wa awali kabla ya mahakama hiyo kuanzisha mchakato wa kumfungulia mashtaka kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha za umma akitumia wadhifa wake huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.