Pata taarifa kuu
UNSC-ADF-Vikwazo

Kundi la waasi wa Uganda ADF lachukuliwa vikwazo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kuliwekea vikwazo kundi la waasi la Uganda la ADF, linaloendesha harakati zake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanadiplomasia wa baraza hilo wamethibitisha.

Conseil de sécurité de l'ONU à New York
Conseil de sécurité de l'ONU à New York REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo, viliyopendekezwa na kamati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulingana na azimio la mwaka 2004, ambalo linaliwekea vikwazo vya vya silaha kundi la ADF na vikwazo vya kusafiri kwa viongozi wa kundi hilo. Wakati huu Ufaransa, Marekani na Uingereza walikua mstari wa mbele kwa kuomba vikwazo hivyo dhidi ya ADF.

Kundi la ADF, ambalo linajulikana kwa jina la ADF-Nalu linatuhumiwa kusajili watoto kama wapiganaji, kutekeleza maovu mbalimbali hususan ubakaji, ukiukwaji wa haki za binadamu, na kuwashambulia wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kifaru cha wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa Monusco, kikijielekeza katika uwanja wa mapigano., Machi 13 mwaka 2014.
Kifaru cha wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa Monusco, kikijielekeza katika uwanja wa mapigano., Machi 13 mwaka 2014. Monusco/Sylvain Liechti

Kundi hilo linaaminika kuwa linaundwa na wanamgambo wa kiislamu, baada ya kiongozi, Jamil Mukulu, na naibu wake, Hood Lukwago, kubadili dini na kuwa waislamu. Awali viongozi hao walikuwa waumini wa kanisa katoliki. Mwaka 2001 Marekani ilimuweka, Jamii Mukulu, kwenye orodha ya viongozi wa makundi ya kigaidi. Kiongozi huyo wa kundi la ADF aliwkewa vikwazo na Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2011, huku Umoja wa Ulaya ikimuwekea vikwazo tangu mwaka 2012.

Kundi hili lilianzisha harakati zake tangu mwaka 1995 katika milima ya Rwenzori (kusini magharibi mwa Uganda), huku likijifadhili kupitia biashara ya miti na madini ya aina ya dhahabu.

Mwezi Januari, jeshi la Congo likishirikiana na wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa Monusco waliendesha mashambulizxi dhidi ya kundi la ADF. Mwezi Aprili serikali ya Kinshasa ilfahamisha kuteka ngome ya mwisho ya kundi hilo kaskazini mwa mkoa wa Kivu kaskazini (mashariki mwa Congo), pembezuni mwa mpaka wa Uganda.

Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Lambert Mende, msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. DR

Kabla ya mashambulizi hayo, timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa walikadia kua idadi ya wapiganaji wa kundi la ADF ni kati ya 1200 na 1500, lakini kwa sasa idadi hio imepungua na kwa asilimia zaidi ya 70.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.