Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-Mgomo

Afrika Kusini: wafanyakazi wa viwanda vya chuma wagoma

Takribani robo milioni ya wafanyakazi wa viwanda vya chuma nchini AfrikaKusini wameweka chini zana za kazi na kuingia katika mgomo hii leo ikiwa ni mwanzo wa mgomo usiokuwa na kikomo.

wa wafanyakazi wa viwanda vya chuma nchini Afrika Kusini waandamana katika miji kadhaa nchini Afrika Kusini.
wa wafanyakazi wa viwanda vya chuma nchini Afrika Kusini waandamana katika miji kadhaa nchini Afrika Kusini.
Matangazo ya kibiashara

Muungano wa wafanyakazi wa viwanda vya chuma nchini Afrika Kusini wameandamana katika miji kadhaa wakidai ongezeko la wastani wa asilimia 10 ya kipato chao, kuboreshewa makazi na marupurupu, madai ambayo wanaamini yatatekelezwa.

Mgomo huu unataraji kuhusisha karibu viwanda elfu kumi vya vyuma na uhandisi ambavyo kwa ujumla vinachangia asilimmia 4 ya uchumi wa Afrika Kusini kulingana na tahmini ya wataalam wa kiuchumi.

Baadhi ya makampuni ya kimataifa yataguswa na athari za mgomo huu zikiwemo BAE Systems na Bell Equipment.

Mazungumzo ya mara ya mwisho jana usiku kati ya Muungano wa wafanyakazi na viongozi wa viwanda yalivunjwa na waziri wa kazi Mildred Oliphant aliyeshindwa kufikia makubaliano na wafanyakazi hao.

Migomo hii katika taifa tajiri kwa viwanda barani Afrika inatajwa kudhoofisha uchumi wa taifa hili ikizingatiwa kuwa ni siku chache zimepita tangu kumalizika kwa mgomo katika sekta ya madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.