Pata taarifa kuu
SUDAN

Polisi nchini Sudan wamkamata tena mwanamke aliyekataa kuasi Ukristo

Polisi jijini Khartoum nchini Sudan wamemkamata mwanamke wa dini ya Kikirtso aliyeachiliwa huru siku ya Jumatatu baada Mahakama ya rufaa kufuta hukumu ya kunyongwa iliyokuwa aliyokuwa amehukumiwa kwa kosa la kukana dini ya Kislamu.

Meriam Yahia Ibrahim Ishag, akiwa na mwanaye
Meriam Yahia Ibrahim Ishag, akiwa na mwanaye
Matangazo ya kibiashara

Mwanake huyo Meriam Yahia Ibrahim Ishag mwenye umri wa miaka 26, amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum akijiaribu kuondoka nchini humo.

Duru zinasema Ishag amekamatwa na mumewe Daniel Wani na haijafahamika ni wapi walikopelekwa baada ya kuonekana katika uwanja wa ndege wakiwa na mtoto wao.

“ Maafisa wa usalama wa taifa walimchukua yeye na mumewe Daniel,” aliyeshuhudia kukamatwa kwa wawili hao ambaye hakutaka jina lake kutajwa amelieleza shirika la habari la Ufaransa AFP.

Hukumu dhidi ya Ishag mwezi uliopita ililaaniwa na Jumuiya ya Kimataifa na Mashirika ya kutetea haki za Binadamu yaliyosema hatua ya Mahakama ya Khartoum ilikwenda kinyume na haki za kuabudu.

Meriam akiwa na mme wake Dani
Meriam akiwa na mme wake Dani Reuters

Mbali na Mashirika hayo ya kutetea haki za Binadamu yakiwemo Human Righst Watch na Amnesty International, zaidi ya watu Milioni moja walitumia tovuti ya Change.org kuendelea na shinikizo za kutaka kuachiliwa kwa mwanamke huyo.

Babake Ishag alikuwa Mwislamu na mamake Mkiristo wa dhehebu la Orthodox kutoka nchini Ethiopia na hatua yake ya kutaka kuolewa na Mkiristo ilimletea matatizo na kukataa kuikana dini yake.

Mahakama ilikuwa imemhukumu kunyongwa kutokana na sheria ya Kiislamu ya mwaka 1983 kuwa mtu hastahili kuikana dini ya Kiislamu na hukumu yake ni kifo.

Ishag alipokuwa na umri wa miaka mitano, babake yake ambaye alikuwa Mwislamu aliiacha familia yake na akalelewa kwa misingi ya dini ya Kikiristo upande wa mamake.

Mwanamke huyo ambaye alijiifungulia jela, alikuwa anatoroka Sudan kwa kuhofia usalama wake baada ya kuachiliwa huru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.