Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Mwandishi wa Habari ashikiliwa na polisi nchini Zimbabwe.

Polisi nchini Zimbabwe wanamshikilia mhariri mkuu wa gazeti la Serikali la sunday Mail, Edmund Kudzayi, ikiwa ni miezi miwili tu toka mhariri huyo alipoteuliwa kushika wadhifa huo.Hata hivyo, inaarifiwa kwamba kushikiliwa kwa mwandishi huyo wa habari huyo kunaambatana na sababu za kisiasa.

Mhariri wa Gazeti la Serikali la Sunday Mail nchini Zimbabwe Juni 19 2014
Mhariri wa Gazeti la Serikali la Sunday Mail nchini Zimbabwe Juni 19 2014 Sunday Mail/News paper
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mhariri msaidizi wa gazeti hilo, amesema kuwa polisi walivamia ofisi za Edmund na kuchukua baadhi ya vifaa zikiwemo laptop na vifaa vingine ambavyo havikufahamika mara moja.

Toka achukue jukumu hilo miezi miwili iliyopita, Edmund amekuwa mkosoaji mkubwa wa wanasiasa wa ndani ya chama tawala ambao wamekuwa wakitofautiana kuhusu uongozi wa rais Robert Mugabe.

Mwezi mmoja uliopita rais Mugabe alimtuhumu waziri wake wa habari, Jonathan Moyo kutumia madaraka yake vibaya kwa kuchochea magazeti ya Serikali kuandika habari mbaya kuhusu wanasiasa wa chama tawala cha ZANU-PF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.