Pata taarifa kuu
New York

Ban Ki Moon: Ajira kwa vijana ni kero katika dunia nzima

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa nchi zote duniani kutafuta mbinu ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira hasa miongoni mwa vijana.Moon amezitaka serikali mbalimbali kuanzisha miradi itakayowasadia vijana kupata kazi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao na rais wa kamati ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao na rais wa kamati ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Hili ni tatizo katika nchi za Afrika Mashariki na nchini Tanzania, hatua ya Wizara ya Mambo ya ndani kuwataka zaidi ya raia elfu kumi wa nchi hiyo kufanya usaili wa kazi 70 inaelezwa na watalaam wa maswala ya ajira na uchumi nchini humo inaashirikia hatari ya kuwepo kwa bomu la ukosefu wa ajira ambalo huenda likalipuka ikiwa halitashughilikiwa.

Ukosefu wa ajira umewafanya vijana wengi pia katika afrika ya kati hususan nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, na Burundi, kujiunga na makundi yenye kumiliki silaha, hali ambayo inakithiri sana katika nchi hiyo, kwa muda wa miongo kadhaa.

Shirika la kazi dunia,. ILO linasema zaidi ya vijana Milioni 70 kwa sasa hawana kazi na wengine zaidi ya 200 wanafanya vibaruia ambao haviwasaidii.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.