Pata taarifa kuu
KENYA

Raisi Uhuru kenyatta akiri kuwa Mauaji ya Mpeketoni yalichochewa na mtandao wa Kisiasa

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Hii leo jumanne amekanusha kuwa kundi la Alshabab lilihusisha na mauaji yaliyotekelezwa katika mji wa Mpeketoni, pwani ya Kenya hivi majuzi na kusema kuwa ni shambulizi lililochochewa na mitandao ya kisiasa ndani ya taifa hilo.Kauli ya raisi Kenyatta inakuja siku moja baada ya kundi la wapiganaji wa al-shabab kukiri kuhusika na shambulio hilo, kama shinikizo dhidi ya serikali ya kenya kuwatoa wanajeshi wake huko Somalia.

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akizungumza wakati wa sherehe za madaraka day juma hili
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akizungumza wakati wa sherehe za madaraka day juma hili Kenyagvt
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia televisheni moja mjini Nairobi nchini Kenya, raisi Uhuru Kenyatta amesema kwamba kuna ushahidi kuonyesha kuwa shambulizi hilo lilipangwa vyema nchini humo na kwamba wanasiasa walihusika nao kwa kuwa walishiriki katika maandalizi na utekelezwaji wa uhalifu huo wa kutisha.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotrolewa jana Jumatatu jioni Kundi la Al Shabab lenyewe lilikiri kuwa ndilo lililotekelezwa mauaji hayo katika mji wa Mpeketoni baada ya kuvizia vituo muhimu vya polisi na mahoteli yanayowavutia watalii.

Kenyatta amesema kuwa vyombo vya dola vilipewa taarifa kuwa mashambulizi hayo yangefanyika lakini kilichoonekana hawakuchukua hatua zozote kuzuia mashambulizi hayo.

Maafisa wakuu wa mashirika ya ujasusi waliohusika tayari wameachishwa kazi na kwamba watashitakiwa mbele ya mahakama.

Hata hivyo Raisi Kenyatta amesema kuwa maafisa wakuu wa kijeshi na wengine kutoka vyombo vya dola wanachunguza wanasiasa waliohusika na mauaji hayo.

Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketoni walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.