Mpinzani mwingine akamatwa nchini Sudan
Polisi nchini Sudan jana imemkamata kiongozi mwingine wa upinzani nchini humo Ibrahim al-Sheikh wakimtuhumu kutoa hotuba ya kichochezi wakati alipofanya mkutano wa hadhara magharibi mwa jimbo la Kordofan.
Imechapishwa:
Ibrahim al-Sheikh ambaye ni kiongozi wa chama cha Sudanese Congress alikamatwa akiwa nyumbani kwake na maofisa wa Polisi ambao walidai wanamshikilia kwa mahojiano kutokana na matamshi yake aliyoyatoa wakati wa mkutano wa kisiasa.
Kiongozi huyo wa upinzani aliyekamatwa mjini Nouhoud kitongoji kilichokopo Kordofan magharibi, huenda akakatiwa adhabu ya kifo iwapo atakutikana na makosa
Kukamatwa kwa Ibrahim al-Sheikh kunakuja ikiwa yamepita majuma kadhaa toka kiongozi mwingine wa kisasa na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa taifa hilo, Sadiq al-Mahdi kukamtwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi kwenye jimbo la kordofan.
Wanasiasa nchini humo wanaona kuwa huu ni mpango wa Serikali ya rais Omar al-Bashir kutaka kudhoofisha upinzani na kwamba hata viongozi hao wakiachiwa hali haitabadilika.