Pata taarifa kuu
DRC-MASHIRIKA YA HAKI ZA BINADAMU-Sheria

Mahakama ya kijeshi nchini DRC yashushiwa lawama

Mashirika mbalimbali ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu duniani yameeleza kuguswa na hukumu iliyotolewa juma hili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, ambapo mahakama ya kijeshi iliwahukumu wanajeshi wawili pekee kati ya 39 waliokuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya ubakaji kwenye mji wa Minova.

Mmoja kati ya majaji wawili katika kesi ya wanajeshi 39 waliyokua wakituhumiwa makosa ya ubakaji katika mji wa Minova akikumbusha adhabu iliyoombwa na muendeshamashitaka mkuu wa taifa.
Mmoja kati ya majaji wawili katika kesi ya wanajeshi 39 waliyokua wakituhumiwa makosa ya ubakaji katika mji wa Minova akikumbusha adhabu iliyoombwa na muendeshamashitaka mkuu wa taifa. RFI/Lea Westerhoff
Matangazo ya kibiashara

Mashirika haya likiwemo lile la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na watoto UNHCR yanasema kuwa hii ni wazi inaonesha kwanamna gani haki imekuwa ngumu kupatikana kwa wanawake ambao walifanyiwa vitendo vya ubakaji na wanajeshi wa serikali, jambo ambalo linakatisha tamaa.

Kwa upande wake shirika la Enough Project nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linasema kuwa kukosekana kwa ushahidi, kushirikiana na nyezo za kufanya uchunguzi wa kina ndivyo vilivyosababisha majaji wa mahakama hiyo ya kijeshi kutowakuta na hatia wanajeshi wengi waliokuwa wanashtakiwa.

Hukumu hii imetolewa huku mamia ya wanawake waliobakwa mashariki mwa nchi hiyo wakati wa vita wakiendelea kuilaumu serikali kwa kushindwa kuthibitisha makosa yaliyokuwa yanawakabili wanajeshi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.