Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Nigeria yapoteza watu 71

Watu 71 wameuawa mapema leo asubuhi na wengine 124 wamejeruhiwa katika mashambulizi tofauti ya mabomu yaliyotokea kwenye kituo cha magari, nji kidogo na mji wa Abuja, ploisi imethibitisha.

Kituo cha magari kilioko eneo la Nyanya, nje kidogo na mji wa Abuja, ambacho kimelengwa na mashambulizi mawili mfululizo.
Kituo cha magari kilioko eneo la Nyanya, nje kidogo na mji wa Abuja, ambacho kimelengwa na mashambulizi mawili mfululizo. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

“Watu 71wameuawa na wengine 124 wamejeruhiwa. Majeruhi wanahudumiwa kimatibabu katika hospitali ziliyo mikoani na pembezuni mwa mji wa Abuja”, msemaji wa polisi Frank Mba, amesema katika mkutano na waandishi wa habari katika eneo la tukio.

Wakati huohuo, rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameahidi kwamba taifa lake huenda likakumbwa na machafuko ya umwagaji damu yanayotekelezwa na wanamgambo wa kislamu wa kundi la Boko Haram. Rais goodluck Jonathan ameyasema hayo wakati alipokuakidhuru eneo latukio, ambako watu 71 wameuawa.

“Tumepoteza idadi kubwa ya watu”, amesema rais Jonathan wakati alikua katika eneo la tukio liliotokea kwenye kituo cha magari kilioko eneo la Nyanya, nje kidogo na mji wa Abuja. “Kundi la Boko Haram tangu kitambu, lilionekana kwamba ni kizuizi katika maendeleo ya Nigeria (...) lakini tutakabiliana nalo (...) suala la Boko Haramu ni la muda”, amesema rais Goodluck Jonathan.

Taifa la Nigeria limekua likikumbwa mara kwa mara na na mashambulizi ya mabomu, na kusababish vfo vingi, na watu wengine kujeruhiwa.

Mwaka wa 2010 gari liliyobeba vilipuzi lililipuka na kuua watu 12 na wengine 38 kujeruhiwa karibu na eneo la Eagle Square, ambako zilifanyika sherehe za miaka 50 za uhuru wa Nigeria.

Kundi linalotetea kujitenga kwa jimbo la Niger Delta (mend) lilikiri kuhusika na shambulio hilo la kwanza kutokea katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Tangu wakati huo taifa hilo likabiliwa na mashambulizi ya hapa na pale na kusababisha  vifo.

Watu zaidi ya 500 wanaarifiwa kuuawa katika mashambulizi kama hayo tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.