Pata taarifa kuu
Juba-utulivu

Hali ya utulivu imerejea jijini Juba baada ya mapigano ya wanajeshi yaliogharimu maisha ya watano

Hali ya utulivu imerejea jijini Juba baada ya hapo jana kutokea mapigano yaliogharimu maisha ya wanajeshi watano  katika kambi kuu ya kijeshi  nchini Sudan kusini ambapo kumekuwa na mvutano mkali ndani ya jeshi la taifa hilo kukabiliana na kuibuka kwa uasi.

Mwanajeshi wa Sudani Kusini
Mwanajeshi wa Sudani Kusini AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Mirindimo ya risasi ilisikika katika kambi hiyo iliyopo jirani na chuo kikuu cha juba na makazi ya walinzi wa raisi kwa takribani saa 2 hivi.

Serikali inalalamikiwa kuchangia vurugu hizo kutokana na kutokuelewana juu malipo ya wanajeshi ambapo Msemaji wa Jeshi Malak Ayuen aliiambia AFP askari watano waliuawa na kwamba wakaopatikana kuhusika na mauaji watashughulikiwa na mahakama ya kijeshi.

Msemaji huyo alibainish akuwa ni kutokuelewana baina ya makomandoo juu ya masuala ya malipo na jambo hilo limeishiia katika kitengo chao.

Sudani Kusini iliingia katika mzozo tangu Desemba 15 mwaka jana, ambapo mapiganao yanashuhudiwa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi tiifu kwa makam wa kwanza wa zamani wa serikali Riek Mashar.

Mapigano hayo yalianzia mjini Juba kabla ya kutanda katika miji mingine nchini humo. Maelfu wa watu wanaripotiwa kupoteza maisha huku takriban watu laki tisa wakiyatoroka makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.