Pata taarifa kuu
RWANDA-Sheria

Rwanda : Kesi ya watuhumiwa 16 wa milipuko mjini Kigali yaendelea

Kesi ya ugaidi inayomhusisha aliyekuwa mlinzi wa rais Paul Kagame, Joel Mutabazi na wenzake 15 inaendelea jijini Kigali. Kesi ambayo wizara ya ulinzi ya Rwanda imeita “kesi ya ugaidi” , inaingia leo kwa siku ya tatu, ambapo watuhumiwa kumi na sita wakiwemo wanajeshi wazamani wa Rwanda Joel Mutabazi na Innocent Kalisa wanatuhumiwa kujiunga na chama cha RNC cha Patrick Karegeya aliyekuwa mkuu wa intelijensia wa Rwanda katika miaka ya 1994 na 2005 ambae aliyeuawa mapema mwaka huu nchini Afrika Kusini.

Moja ya maeneo ya matukiyo ya milipuko ya gruneti, mjini Kigali
Moja ya maeneo ya matukiyo ya milipuko ya gruneti, mjini Kigali RFI
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Rwanda jenerali Joseph Nzabamwita amesema kuwa serikali ina uhakika kesi hii itasaidia kuonesha ushirikiano wa kiuhalifu ulioko kati ya chama cha RNC, na waasi wa Kihutu wa FDLR.

Wakati hayo yakijiri, ripoti ya shirika la kutetea Haki za Binadamu la Human Right Watch limeelezea wasiwasi wake kuhusiana na mfululizo wa mauaji ya kisiasa ya wapinzani wa Rwanda na kuiomba serikali ya rais kagame kutoa ushirikiano kwa uchunguzi.

Mwakilishi wa Human rwight Watch katika ukanda wa maziwa Makuu, Carina Tersakian ameomba serikali ya Kigali itowe ushirikiano wa kutosha iwapo itaombwa kufanya hivo kuhusu chunguzi hizo.

“Hukohuko nchini Rwanda palikuwepo na matukio ya kuwashambulia wapinzani, kuwakamata na kuwafungulia mashtaka, kwa hiyo kuna hali kama ya giza hivi, hali ya kukosa uvumilivu kwa wote ambao wanajaribu kukosoa kwa njia ya siasa.

Kwa hiyo tunaomba serikali za nchi ambako mashambulizi hayo yametokea kufanya chunguzi za kina, na tunaomba serikali ya rwanda kutoa ushirikiano wao kwa viongozi wa kisheria wa nchi husika”, amesema Carina Tersakian.

Wakati huohuo, Shirikisho la Kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la FIDH limeelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ufunguzi wa kesi ya kwanza ya mauaji ya kimbari ya Rwanda katika ardhi ya Ufaransa tarehe 4 Februari.

Patrick Baudoin, rais wa heshima wa FIDH amesema kesi za mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu zimekua zikishughulikiwa kwa kina, akibaini kwamba kuna maendeleo katika haki za binadamu.

“Yako maendeleo hususan uundwaji wa jopo la wataalam wa uhalifu wa kivita, dhidi ya haki za binadam na mauwaji ya kimbari, na jopo hiyo inashirikisha mahakimu waliobobea katika kesi nyingi za wanaotuhumiwa kufanya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda”, amesema Baudoin.

Claude Munyamana, mmoja wa watuhumiwa wa mauwaji hayo aishiye nchini Ufaransa anaelezea utayari wake kukabiliana na mashtaka hayo na kutipilia mbali shutuma hizo.

“Nchini Rwanda hakuna utawala wa sheria, mimi sina hatia, tarehe zinazotajwa kwa ajili ya mauwaji hayo mimi sikuwepo kwenye eneo husika, nilikuwa katika eneo lingine.

Suala liliopo hapo ni kwamba mwaka 1994, mimi ndiye niliyekuwa nawaongoza askari wa Ufaransa, niliombwa kutia saini waraka unaowatuhumu askari hao waliokuwepo mkoani Kibuye, nilikataa na ndiyo maana nilikimbia nchi yangu mwaka wa 95, amesema Munyamana.

Serikali ya Kigali imekua iwanyooshea kidole wapinzani wake waishio ugenini kwmba wamekua wakichochea uhasama na vurugu nchini Rwanda, tuhumba ambazo zinatupiliwa mbali na wapinzani wa utawala wa Paul Kagame, wakibaini kwamba utawala huo una lengo la kuangamiza wapinzani.

Hivi karibuni mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda, ambae alikua pia mshirika wa karibu wa rais Paul Kagame, Kayumba Nyamwasa, ambae yuko ukimbizini chini Afrika Kusini, aliutuhumu utawala wa Kagame kwamba ulihusika katika kifo cha Patrick Karegeya.

Patrick Karegeya, ambae alikua mkuu wa idara ya ujasusi nchini Rwanda katika miaka ya 1994 hadi 2005, alikutwa ameuawa katika hoteli moja mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.