Pata taarifa kuu
MISRI-Kura ya maoni

Raia nchini Misri wapitisha katiba mpya kwa asilimia 98.1

Wapiga kura nchini Misri wamepitisha katiba mpya kwa asilimia 98.1, mkuu wa uchaguzi amesema jana Jumamosi, katika kile ambacho Serikali imetangaza kuwa ni kuunga mkono hatua ya jeshi kumpindua rais Mohamed Morsi.

Raia wa Misri wakifurahia matokeo ya kura ya maoni
Raia wa Misri wakifurahia matokeo ya kura ya maoni www.latimes.com
Matangazo ya kibiashara

Matokeo hayo ya kura ya maoni iliyofanyika Jumanne na Jumatano juma hili,hayakutiliwa shaka kamwe ,wakati wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood na vyama vingine vya kiislam, walipogomea kura hiyo, lakini mamlaka ilitaka mwitikio mkubwa katika jaribio hilo la kwanza la demokrasia tangu kung'olewa kwa Morsi mwezi Julai.

Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Sisi, jenerali ambaye aliongoza mapinduzi ya Morsi, alikuwa akifuatilia matokeo ili kupata ishara ya kuunga mkono uwezekano wa jitihada za urais, maafisa wa kijeshi wamesema.
Afisa wa juu wa serikali amesema kuwa mwitikio huo wa watu wengi umethibitisha uhalali wa mapinduzi ya June 30 ambapo katiba hiyo mpya inachukua nafasi ya katiba iliyopitishwa mwezi Disemba mwaka 2012 chini ya rais Morsi, ambapo ilipata theluthi mbili ya kura zote huku asilimia 33 ya raia wakijitokeza kupiga kura.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.