Polisi watano na raia wawili wauawa katika shambulizi mpakani mwa Kenya na Somalia
Polisi watano na raia wawili wameuawa katika shambulizi dhidi yao lililofanywa na watu waliojihami kwa silaha kwenye mpaka wa Kenya na Somalia,jeshi la polisi nchini kenya limethibitisha.
Imechapishwa:
Shambulizi hilo limefanyika katika barabara iliyoko kati ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ya Dadaab na mji wa Mashariki wa Liboi wakati askari hao walipokuwa wakishika doria .
Taarifa zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa polisi wengine wawili bado hawajulikani walipo kufuatia tukio hilo.
Mpaka wa Kenya na Somalia umekuwa kitovu cha mashambulizi ya kuvizia yanayofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab pamoja na makundi mengine ya watu waliojihami.