Pata taarifa kuu
DRCONGO-MONUSCO-M23

Kesi ya wanajeshi wa serikali ya DRC wanaotuhumiwa kwa ubakaji na mauaji imeanza kusikilizwa jana mjini Goma

Kesi inayowakabili watuhumiwa 39 wa ubakaji Kutoka jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeanza kusikilizwa jana Mjini Goma, mashariki mwa Nchi hiyo. 

Wanajeshi wa FARDC
Wanajeshi wa FARDC RFI / Léa-Lisa Westerhoff
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao wa Jeshi la serikali ya Congo FARDC wanatuhumiwa kuhusika katika vitendo vya ubakaji, mauaji pamoja na uporaji wa mali ya raia katika mji wa Minova huko Kivu ya Kaskazini, na kuendesha vitendo vya unyanyasaji wakati wa mapigano kati yao na Kundi la waasi wa zamani wa M23.

Hata hivyo watuhumiwa hao wamekanusha kuhusika katika vitendo hivyo, jambo ambalo limemfanya mwanasheria wa upande wa utetezi Sylvestre Bissimwa kueleza kuwa kuna dalili zinazoonyesha kuhusika kwao katika Vitendo hivyo.

Wananchi wa DRC na wale wa nchi rafiki wa Congo,wameiomba mahakama ya kijeshi inayosikiliza kesi ya wanajeshi hao kutenda haki ili kukomesha vitendo hivyo vya kikatili nchini humo na kuwatia moyo waathirika wa vitendo hivyo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.