Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Zuma ajikuta kikaangoni baada ya utajiri wake uliokithiri kubainishwa

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amejikuta katika wakati mgumu baada ya kubainika kuwa alifaidika binafi na ukarabati tata wa masuala ya usalama nyumbani kwake na hivyo analazimika kulilipa taifa hilo , shirika moja limevujisha taarifa hizo kwenye gazeti moja nchini humo. Leo Ijumaa. 

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Serikali imetumia takribani randi milioni 200 sawa na dola milioni 20 kufufua vijijini vya nyumbani kwao Zuma ikiwa ni pamoja na bwawa la kuogelea na jengo la michezo ya jukwaani,na kulihalalisha kama sehemu ya muhimu kwa usalama kwa ajili ya mkuu wa nchi.

Lakini shirika la serikali katika ripoti yenye jina la 'Opulence on Grand Scale likimaanisha utajiri uliokithiri, limegundua kwamba Zuma alipata faida kubwa kupitia mpango huo,gazeti la kila siku la nchini Afrika Kusini Mail & Guardian limeripoti.

Ripoti za wakaguzi wa mali za umma nchini humo zimearifu kuhusu matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na viongozi ,na kuchapisha matokeo ya utafiti, na kutoa mapendekezo ya kufunguliwa mashtaka dhidi yao pale inapohitajika.
mashtaka ambapo inahitajika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.