Pata taarifa kuu
BURUNDI

Serikali ya Burundi yakubali kufanya marekebisho ya katiba kwa kushirikiana na wanasiasa wa upinzani

Hatimaye serikali ya Burundi imekubali kuendeleza mchakato wa kuifanya marekebisho ya katiba kwa kushirikiana na wanasiasa hususan wale wa upinzani baada ya majadiliano ya jana kati ya serikali, wanasiasa wa chama tawala na wale wa upinzani. 

Makamu wa kwanza wa rais wa Burundi Bernard Basokoza
Makamu wa kwanza wa rais wa Burundi Bernard Basokoza thehabari.com
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa kwanza wa rais wa Burundi, Bernard Basokoza, amesema serikali yake iko tayari kwa majadiliano juu ya baadhi ya vipengele vya katiba vinavyo hitaji kurekebishwa.

Hata hivyo Basokoza, amesema msimamo huo mpya wa serikali unalenga kuandaa mazingira mazuri yatakayoruhusu uchaguzi wa mwaka 2015 kuwa huru na wazi, kauli ambayo upinzani nchini Burundi unasema kuwa una mashaka nayo.

Katika hatua nyingine muungano wa vyama tisa vya upinzani nchini Burundi ADECEE-Ikibiri umeandaa maandamano ya kushinikiza serikali ili kufanya mjadala wa marekebisho ya katiba kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Kwa mujibu wa msemaji wa vyama hivyo Chovinoo Mugwengezo, tayari vyama hivyo vilishatoa notisi kwa serikali juu ya maandamano hayo

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.