Pata taarifa kuu
TUNISIA

Waandamanaji nchini Tunisia wachoma moto ofisi za chama tawala

Mamia ya waandamanaji nchini Tunisia wamechoma moto ofisi za chama chama tawala nchini humo, katika mkoa uliosahaulika wa Gafsa, moja ya maeneo kadhaa yaliyo kwenye mgomo.

Waandamanaji nchini Tunisia
Waandamanaji nchini Tunisia REUTERS/Anis Mili
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji wamevamia makao makuu ya ofisi za chama cha Ennahda huko Gafsa katkati mwa Tunisia, baada ya kujaribu kuingia kenye ofisi za gavana wa mkoa ambapo walitawanywa na polisi.

Waandamanaji hao wamechukua mafaili na samani kutoka katika ofisi hizo na kuzichoma moto barabarani , huku wakiwazuia watu wa zima moto kufika katika jengo hilo

Mgomo huo umeitishwa kupinga hali ya umasikini na ukosefu wa maendeleo,mambo ambayo yalisababisha kutokea kwa machafuko yaliyomwondosha madarakani rais wa nchi hiyo Zine El Abidine Ben Ali mnamo mwezi Januari mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.