Pata taarifa kuu
DRC

Wapinzani nchini DRCongo waunda muungano mpya kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2016

Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini DRCongo wameunda muungano mpya uliobatizwa jina la ''Tuiokoe Congo'' kwa ajili ya kujiandaa na uchaguzi mkuu wa rais wa mwaka 2016. Kulingana na mmoja kati ya viongozi hao Martin Fayulu amesema lengo la muungano huo ni kudumisha demokrasia na kuhakikisha uchaguzi wa wajumbe wa baraza la seneti na serikali za mitaa unafanyika mwaka 2014 na 2015 kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2016.

Matangazo ya kibiashara

Rais Joseph Kabila yupo madarakani nchini DRCongo tangu mwaka 2001 na alichaguliwa tena kuendelea kuliongoza taifa hilo mwaka 2011 katika uchaguzi ambao ulipingwa vikali na upinzani na hivyo kuzua mzozo wa kisiasa, hali iliyosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa wajumbe wa baraza la Seneti, magavana na viongozi wa serikali za mitaa.

Hata hivyo vyama vikuu viwili vya upinzani kile cha UDPS cha Etienne Tschisekedi na kile cha UNC cha Vital Kamerhe vimejiweka kando na muungano huo.

Wabunge kutoka muungano wa vyama vinavyounga mkono utawala wa rais Joseh Kabila wao wanaona kwamba muungano huo hauna lolote, na kwamba rais Kabila ndiye mkombozi wa raia wa nchi hiyo.

Hivi karibuni rais Kabila alitangaza kuunda Tume itakayosimamia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyofanyika nchini humo.

Katika hotuba yale iliyohitimisha mnazungumzo hayo, rais Kabila aliahidi uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa itakayojumuisha wadau kutoka pande zote hasa vyama vya upinzani.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimetupilia mbali pendekezo hilo na kubainisha kuwa kilicho cha muhimu kwa sasa ni kuweka misingi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 kwa vile rais huyo anaelekea mwishoni mwa muhula wake wa pili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.