Pata taarifa kuu
PUNTLAND

Raia wawili wa kigeni wakamatwa kwa tuhuma za kupeleleza siri za serikali ya eneo lililojitenga na Somalia la Puntland

Serikali ya eneo lililojitenga na Somalia, Puntland imetangaza kuwashikilia raia wawili wa kigeni toka Ufaransa na Uingereza kwa tuhuma za kupeleleza maswala ya Taifa hilo. Waziri wa Ulinzi wa Puntland, Kalif Ise Mudan amesema wanawashikilia watu hao ambao waliingia kama wafanyakazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali NGO's.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mudan amesema wawili hao wamekuwa wakifanya upelelezi kwa muda mrefu na walikamatwa wakifanya wakiendesha shughuli tofauti na zile walizodai wanafanya nchini humo.

Taarifa toka nchini humo zimebaini kuwa watu hao walikuwa wakitafuta taarifa za siri kutoka katika taasisi za serikali na binafsi huko Puntland, na taarifa hizo wamekuwa wakizitoa kwa watu wa nje ya Taifa hilo.

Wafanyakazi wengine wawili raia wa Taifa hilo wanashikiliwa kwa tuhuma za kusaidiana na raia hao wa kigeni.

Serikali ya London imethbitisha kushikiliwa kwa raia wake na kusema inawasiliana na mamlaka za Puntland kuhusiana na suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.