Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Afrika Kusini waanza kusajili wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2014

Wananchi wa Afrika Kusini hii leo wanaanza kushiriki zoezi la usajili wa wapiga kura litakalofanyika kwa siku mbili mfululizo, ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2014 ambao unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka ishirini tangu kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi.

REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Taifa hilo Jacob Zuma amewataka raia wake kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambalo linatarajiwa kufanyika kwa amani na utulivu, huku vyombo vya usalama vikisema vimejidhatiti kuhakikisha hakuna uvunjifu wowote wa amani utakaojitokeza.

Vijana waliozaliwa baada ya mwaka 1994 ambao kwa mara ya kwanza washiriki zoezi hilo baada ya kutimiza umri unaoruhusiwa, wamehimizwa kujitokeza zaidi na kuchaguzi viongozi wao.

Zuma ambaye anatarajiwa kuwania tena Urais katika uchaguzi ujao kupitia chama tawala cha ANC amesema anatarajia uchaguzi ujao utaendeleza historia nzuri katika utawala wa kidemokrasia ndani ya Taifa hilo.

Hata hivyo umaarufu wa kiongozi huyo na chama chake kilichokumbwa na migogoro na utadhihirika hapo mwakani atakapochuana na Julius Malema ambaye alitimuliwa kutoka katika chama hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.