Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI

Viongozi wa juu wa Al-Shabab wauliwa kwa kushambuliwa na ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani

Viongozi wawili wa juu wa kundi la kigaidi la Al Shabab nchini Somalia wameuawa baada ya msafara wao kushambuliwa na ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani katika mji wa Jilib.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za serikali ya Marekani zinasema kuwa mmoja wa kiongozi wa kundi hilo aliyeuawa alikuwa mtaalam wa kurusha mabomu na aliuawa pamoja na watu wengine wawili.

Mwanachama wa Al- Shabab aliyejitambulisha kwa jina la Abu Mohamed amesema kuwa aliyeuawa anafahamika kwa jina la Anta na alikuwa mtaalam wa kurusha mabomu.

Taarifa za Kiilnteljensia zinasema kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa baada ya wanamgambo hao wa Al Shabab kuwa katika harakati za kwenda kusuluhisha mgogoro wa kijamii.

Mapema mwezi huu, wanajeshi wa Marekani walijaribu bila mafanikio Pwani ya Somalia kujaribu kumuua kiongozi wa juu wa Al-Shabab na kupata upinzani mkali kutoka kwa wanamgambo hao.

Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Marekani limekuwa likimsaka Abdulkadir Mohamed Abdulkadir, anayefahamika kwa jina lingine kama Ikrima kwa kuongoza mashambulizi ya kigaidi katika jengo la kibiashara la Westgate jijini Nairobi mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 67.

Marekani imeendelea kutumia ndege zisizokuwa na rubani kuwalenga wanamgambo wa Al- Shabab na mwaka 2008 ilifanikiwa kumuua Kamanda wa wanamgambo hao Aden Hashi Ayro.

Marekani imeweka kambi kubwa ya kijeshi katika nchi ya Djibouti karibu na Somalia kupambana na Al-Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.