Pata taarifa kuu
UGANDA

Uganda yaadhimisha miaka 51 ya Uhuru

Uganda inaadhimisha miaka 51 ya uhuru baada ya kutawaliwa na wakoloni kutoka nchini Uingereza miaka ya 1950 na 1960.

Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho hayo yanafanyika huku taifa hilo likikabiliwa na changamoto mbalimbali kufikia malengo ya wananchi wa Uganda.

Hali ya Usalama imeimarishwa jijini Kampala na maeneo mengine katika maadhimisho yanayoongozwa na rais Yoweri Museveni wakati huu wananchi wakilalamika kupanda kwa maisha na hali ya wasiwasi kuhusu usalama wao.

Wanaharakati nchini Uganda wamekuwa wakiandamana jijini Kampala na miji mingine kulalamikia kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu kama sukari, unga na vyakula vingine.

Kuwepo kwa majeshi ya nchi hiyo nchini Somalia pia kunafanya wananchi nchini humo kuhofia usalama wao kutokana na vitisho ya mara kwa mara kutoka kwa kundi hilo la kigaidi ambalo linataka Uganda kuondoa jeshi lake nchini humo.

Mchambuzi wa siasa za Uganda Francis Wambete ambaye pia ni Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Makerere ameimbia RFI Kiswahili kuwa rais Museveni ambaye ameongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 sasa ana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa uchumi wa taifa hilo unakuwa na demokrasia inaimarishwa.

Wambete ameongeza kuwa oparesheni ya mara kwa mara inayofanywa na polisi wa Uganda dhidi ya wapinzani inaonesha wazi kuwa serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata nafasi ya kujieleza.

Kwa mara ya kwanza rais Museveni na mpinzani wake Kizza Besigye watakutana katika sherehe hizo za kitaifa zitakazofanyika katika viwanja vya Rukungiri Magharbi mwa nchi hiyo.

Besigye ambaye amekuwa mpinzani wa rais Museveni katika Uchaguzi Mkuu nchini humo kwa mihula mitatu iliyopita amethibitisha kuhudhuria sherehe hizo baada ya kualikwa na serikali.

Mapema juma hili akiwa jijini Kampala, rais Museveni aliukosoa upinzani ukiongozwa na Besigye kujaribu kupanga mikakati ya kusababisha maandamano makubwa nchini humo kama ilivyoshuhudiwa nchini Misri.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.