Pata taarifa kuu
MALI

Waasi waendeleza mashambulizi Kaskazini mwa Mali

Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa Kaskazini mwa nchi ya Mali katika eneo linalotawaliwa na waasi wa Kislamu wanaoendeleza mashambulizi kuwalenga raia wa kawaida baada ya kudai kuwa serikali imekataa kutekeleza mkataba wa amani walioafikiana nchini Burkinafaso.

Matangazo ya kibiashara

Waasi hao wa Kislamu siku ya Jumanne walitekeleza shambulizi katika daraja moja mjini Gao na kuwajeruhi raia wawili, wakati wa makabiliano yao na jeshi la serikali yakiendelea.

Suala la Ukosefu wa usalama Kaskazini mwa Mali linasalia changamoto kubwa kwa serikali ya rais Ibrahim Boubacar Keita ambaye aliapishwa mwezi uliopita baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika katikati ya mwaka huu.

Rais Keita anasema kazi yake kubwa kipindi hiki ni kuhubiri amani na kuweka mikakati ya kuwapatanisha tena wananchi wa Mali hasa wale wa Kaskazini na kuhakikisha kuwa taifa hio haligawanyiki .

Mjini Gao Polisi wamethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo ambalo limetokea Kilomita 50 karibu na nchi ya Niger.

Kuanzia mwishoni mwa mwezi uliopita, hali ya wasiwasi ilianza kushuhudiwa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya waasi wa Tuareg kuanza kukabiliana na jeshi la serikali.

Waasi hao wamesema hawatarudi tena katika meza ya mazungumzo baada kwa madai kuwa serikali ya Bamako imeshindwa kutekeleza maazimio waliyoafikiana nchini Burkinafaso ya kutaka serikali kuwaachilia huru waasi wote wanaozuiliwa.

Majeshi ya Ufaransa yapatao 4,000 yaliingia nchi Mali kukabiliana na waasi hao na kusaidia kuleta utulivu katika eneo la Azawad ambalo waasi wa Tuareg na makundi mengine yanataka kujitenga .

Paris inasema kuwa itawarudisha nyumbani wanajeshi wake 3,000 kufikia mwisho wa mwaka huu na kuwaacha wengine 1,000 kuendelea kutoa mafunzo kwa jeshi la Mali.

Mbali na jeshi la Ufaransa, jeshi la Umoja wa Afrika chini ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa MINUSMA pia linaendeleza harakati za kulinda amani nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.