Pata taarifa kuu
KENYA

Serikali ya Kenya yasema shambulio la Westgate halijatikisa uchumi wake

Serikali ya Kenya imesema kuwa shambulio la kigaidi katika jumba la biashara la Westgate halijaathiri mipango ya nchi hiyo kuogeza karibu dola bilioni 1.5 katika suala la makubaliano ya ubia wa kimataifa. 

Katibu wa hazina nchini Kenya Henry Rotich
Katibu wa hazina nchini Kenya Henry Rotich en.africatime.com
Matangazo ya kibiashara

Kenya inatafuta nafasi kubwa katika masoko ya kimataifa ili kufufua miundo mbinu ya tangu kipindi cha ukoloni ambayo kwa sasa imeharibika na kuongeza kasi ya uchumi ambao umeporomoka.

Mpango huo wa ubia wa kimataifa ambao utakuwa wa kwanza mkubwa katika taifa hilo la ukanda wa jangwa la Sahara umepangwa kufanyika baadaye mwezi Novemba.

Katibu wa Hazina nchini humo Henry Rotich amesema kuwa uchumi wa Kenya kama ilivyo ari ya watu wake haujatikiswa na janga hilo la hivi karibuni na kwamba msimamo wake katika mpango wa ubia uko palepale.

Wanamgambo wa Al Shabab wenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda wameikejeli Kenya na kutishia kuishambulia zaidi baada ya shambulio la hivi karibuni lililosababisha vifo vya watu zaidi ya sitini huku wengine zaidi ya mia moja wakijeruhiwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.