Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Maelfu ya watu wakimbia makwao Jamhuri ya Afrika ya Kati

Umoja wa Mataifa unasema kuwa maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wameyakimbia makwao katika siku za hivi karibuni kutokana na hofu ya kushambuliwa na makundi ya wapiganaji.

Matangazo ya kibiashara

UN inasema kuwa zaidi ya watu 6,000 wamekimbilia katika uwanja wa ndege wa Bangui wanakopata hifadhi kwa hofu ya kushambuliwa, baada ya baadhi yao kuchomewa maakazi yao.

Wiki kadhaa zilizopita wananchi wa taifa hilo wamekuwa wakilalamikia kuteswa, kukamatwa, kuvamiwa na kuibiwa na makundi ya waasi hali ambayo imeendelea kuhatarisha usalama wa taifa hilo la Afrika ya Kati.

Waasi wa Seleka waliongoza mapinduzi dhidi ya serikali ya rais Francois Bozize mwezi Machi mwaka huu inaongozwa na kiongozi wake Michel Djotodia ambaye amekiri kukabiliwa na changamoto ya ongezeko la visa vya uhalifu nchini humo.

Mepema wiki hii, rais wa Ufaransa Francois Hollande aliitaka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati kupata amani ili nchi hiyo isiwe kama Somalia.

Hollande amesema hali inayoendela nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mbaya sana na ikiwa vifo vya watu vitaendelea kushuhudiwa na wananchi kukimbia makwao nchi hiyo itadhoofika kisiasa na kiuchumi.

Mwezi huu zaidi ya watu 10 walipoteza maisha katika jiji Kuu la Bangui baada ya kutokea kwa makabiliano kati ya wafuasi wa rais wa zamani Francois Bozize na wafuasi wa kundi la Seleka ambalo kwa sasa linaongoza nchi.

Paris inasema kuwa machafuko nchini humo huenda yakawa na matokeo mabaya katika mataifa jirani ya Afrika ya Kati na ikiwa hali ikiendelea kuwa kama ilivyo kwa sasa Umoja wa Mataifa unastahili kutuma jeshi la kulinda amani nchini humo.

Rais Djotodia amekuwa akisema kuwa serikali yake inafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kuhakikisha kuwa usalama unarejea nchini humo kwa kuwapokonya makundi ya waasi silaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.