Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Zimbabwe haina fedha za kutosha kwa ajili ya gharama za uchaguzi

Waziri wa fedha nchini Zimbabwe amesema kuwa bado zimbabwe haina fedha za kutosha kulipa gahrama za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katika kipindi cha miezi mitatu.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe  na waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsvangirai Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi nchini Zimbabwe utafanyika tarehe 31 mwezi Julai huku Rais wa nchi huyi Robert Mugabe akitazamia kumshinda Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai.
 

Baada ya maelfu ya Raia wa Zimbabwe kushindwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapigakura, Waziri wa Fedha Tendai Biti ameomba Mamlaka zinazoshughulikia maswala ya uchaguzi kuongeza muda wa kujiandikisha mpaka juma lijalo.
 

Biti ametoa wito kwa Viongozi wa Jumuia ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kuingilia kati kwa kuwa mabadiliko katika maswala ya Usalama, Vyombo vya Habari na Tume ya uchaguzi bado hayajafanyiwa kazi.
 

Biti amesema huu ni wakati wa SADC kutathimini kama inawezekana kwa Zimbabwe kufanya uchaguzi ulio wa haki.
 

Biti ametoa shutma kwa Chama za ZANU-PF kuwa kimeipa kandarasi Kampuni moja kutoka nchini Israel ili kurubuni uandikishaji wa Wapigakura.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.