Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAREKANI

Rais Obama awasili nchini Tanzania kukamilisha ziara yake Barani Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa zara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.

Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete baada ya kuwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam
Rais Obama akiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete baada ya kuwasili uwanja wa ndege Dar es Salaam
Matangazo ya kibiashara

Obama ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake rais Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe  Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais.

Rais Obama na mwenyeji wake wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya pamoja na kisha Obama atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kabla ya kushiriki dhifa ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali hapo baadaye Ikulu jijini Dar es Salaam.

Aidha hapo kesho Obama atatembelea kituo cha umeme cha Ubungo , baada ya kuahidi kutoa dola za Marekani bilioni saba kusaidia mradi wa umeme Barani Afrika.

Mpango huo wa serikali ya Marekani utazinduliwa kwanza katika nchi za Ethiopia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria na Tanzania ambazo wananchi wake wanakumbwa na matatizo ya upatikanaji wa umeme.

Katika ziara yake Barani Afrika iliyoanzia nchini Senegal, Afrika kusini na hatimaye nchini Tanzania Obama amaekuwa akisisitiza suala la demokrasia ambapo ameeleza kuwa Afrika itakuwa na mustakabali mzuri kwa kuwa na viongozi wanaopambana kuhakikisha raia wao wanakuwa na maisha bora.

Katika ziara yake nchini Afrika Kusini , Obama hakusita kusifu jitihada za kiongozi wa zamani na baba wa taifa hilo Nelson Mandela ambaye ameeleza kuwa jitihada zake za ukombozi kwa raia wa taifa hilo zilimsukuma kuingia katika siasa na hatimaye kuwa rais wa kwanza mweusi nchini Marekani

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.