Pata taarifa kuu
DRCONGO-TANZANIA-RWANDA-UGANDA

Baraza la uratibu shughuli za kijamii mashariki mwa DRCongo latangaza kuunga mkono pendekezo la rais Jakaya Kikwete juu ya Rwanda na Uganda kuzungumza na waasi.

Baraza la uratibu wa shughuli za kijamii mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo linalo jumuisha watu wa makabila la wa Nande, wahunde, wahutu na watutsi, limetangaza uungwaji wake mkono kwa pendekezo lilipoewa kwa nchi za Rwanda na Uganda na Ris Jakaya Mrisho Kikwete Mei 26 iliopita, la kutaka nchi hizo zianzishe mazungumzo na waasi wanaopambana na serikali zao waliopiga kambi mashariki mwa DRCongo.

Viongozi wa kijadi nchini DRCongo
Viongozi wa kijadi nchini DRCongo
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Baraza hilo Jean Sekabuhoro amesema mwishoni mwa juma lililopita kuwa huwezi kulinda nchi yako kwa kuhatarisha usalama wa jirani yako. Kiongozi huyo amesema kuna idadi ya wakimbizi zaidi ya milioni moja walioyatoroka ma kwao, kutokana tu na Rwanda na Uganda ambazo zinawafuatilia waasi katika ardhi ya Congo kwa kutaka kujilindia Usalam.

Jean Sekabuhoro ameendelea kusema kuwa inachosha kuendelea kuvumilia ona nchi ambayo inaweka misingi ya amani yake kwa kuhatarisha uslama na amani ya nchi jirani. Ameitolea wito jamii ya kimataifa kuendeleza shinikizo ili serikali ya Rwanda ielewe ujumbe wa rais Jakaya kikwete.

Katika risala iliotumwa na baraza hilo juma lililopita kwa rais Jakaya Kikwete na kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, baraza hilo linaomba pendekezo hilo la rais wa Tanzania lifuatiliwe na kutekelezwa.

Pendekezo hilo la rais Kikwete lilitolewa wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika na kupokelewa vibaya na Rwanda ambayo haitaki kusikia swala la majadilinao na waasi wa FDLR inayo watuhumu kuhusika na mauaji ya kimbari.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.