Pata taarifa kuu
MALI-KIDAL

Kamati ya mseto yakutana jijini Kidal kwa mara ya kwanza kujadili swala la kuwakusanya wapiganaji.

Kwa mara ya kwanza kamati ya mseto ya usalama imeelekea jijini Kidal jana Juni 23. kamati hiyo ya mseto iliundwa katika mkataba uliosainiwa jijini Burkina Faso na kuundwa na maafisa wanne wa jeshi la Mali, wajumbe wanne wa makundi ya Tuaregs, MNLA na HCUA, wawakilishi wa kikosi maalum nchini Mali Misma na wale wa operesheni ya kijeshi ya Ufaransa, wapatanishi kutoka Burkina Faso pamoja na Ujumbe wa Umoja wa Afrika. Ujumbe huo umebaki jijini hapo muda mchache na hivo kuzua maandamano ya wanawake na vijana.

Kundi la wapiganaji wa Tuareg
Kundi la wapiganaji wa Tuareg REUTERS/Cheick Diouara
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa makundi ya Tuaregs wamesema hawakupewa taarifa kuhusu ujio wa wajumbe hao wa kamati ya mseto kuhusu usalama, lakini hata hivyo haikuzuia wajumbe kukutana kwa mara ya kwanza katika jiji la Kidal. Wajumbe wote wamekutana ili kujadili hatuwa ya kwanza ya kuwakusanya wapiganaji wa MNLA na ujio wa wanajeshi wa Mali.

Kanali Alghaimar wa MNLA ambae ni mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo ya mseto, amefahamisha kuwa kikao hico kilikuwa ni cha kukaguwa idadi ya wapiganaji na silaza zitazo kusanywa, na swala kubwa la maji na umeme tayari limewasilishwa kwa tume hiyo ambayo itawekwa rasmi katika kikao kijacho kitachofanyika katika siku mbili tatu zijazo.

Vituo vingi vyenye hadhi nzuri mathalan vyenye kuwepo maji na umeme sio vingi jijini Kidal ambako kumekuwa na ushindani kati ya wanajeshi wa Mali na wapiganaji wa Tuaregs katika kuwania vituo vilivyo bora zaidi. Pande zote mbili hazijaafikiana kuhusu swala hili.

Mbali na ukusanuaji wa wapiganaji wa Tuaregs na kuwaweka wajaeshi wa mali, kuna swala pia la kuwapatishia nafasi wanajeshi wa kikosi kijacho cha Umoja wa Mataifa nchini Mali (Minusma) ambapo kikosi cha kwanza cha Benin kimeingia jijini Kidal leo kwa ndege na wengine kwa usafuru wa ardhini.

Kuna taarifa za kutoroka kwa wapiganaji wa Tuaregs jijini kidal wakikimbia kukusanywa pamoja kufuatia makubaliano yaliofikiwa jijini Burkina Faso, ambapo kanali Alghaimar amesema hana taarifa hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.