Pata taarifa kuu
SUDAN-SUDAN KUSINI

Khartoum yafunga rasmi mabomba ya kusafirishia mafuta ya Juba

Wizara ya mafuta nchini Sudan inasema kuwa imefunga rasmi mabomba ya kusafirisha mafuta kutoka nchini Sudan Kusini kuzuia mafuta yake kusafirishwa kwa mataifa mengine.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mafuta wa Awad Ahmad al-Jaz ametoa agizo hilo baada ya mkutano wake na Wakurugenzi Wakuu wa kampuni za usafirishaji na kusafisha mafuta.

Khartoum inasema kuwa hatua hiyo itadumu kwa siku sitini zijazo baada ya kuituhumu Juba kuwafadhili waasi wa SPM-N wanaopigana na majeshi ya serikali katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile.

Mapema juma hili serikali ya Sudan ilitangaza kusitisha uhusiano wa kiusalama na kiuchumi na jirani yake Sudan Kusini kutokana na madai hayo ya kuwaunga mkono waasi tuhma ambazo Juba wamepinga.

Khartoum inasema kuwa uhusiano wake na Juba bado utasalia kuwa mzuri ikiwa  Sudan Kusini itaacha kuwaunga mkono waasi kwa kuwapa fedha na silaha, madai ambayo wamesema wamethibitisha kuwa Juba inahusika.

Serikali ya Sudan Kusini inayoongozwa na rais Salva Kiir imeendela kukanusha madai hayop na kuwaomba raia wake kuendelea na maisha yao ya kawaida .

Kiir ameimbia Khartoum kuwa hatua yao ya kufunga mabomba hizo hazitaathiri  uchumi wao na raia wake hawatakufa njaa kwa kile alichokisema kuwa raia wake wamekuwa wakiishi bila ya kutegemea mafuta.

Wachambuzi wa siasa za Sudan wanasema kuwa hatua ya Khartoum ya kusitisha usafirishaji wa mafuta kwa muda wa siku 60, itaathiri uchumi wa Juba ikiwa suluhu la haraka halipatikana kati ya nchi hizo mbili.

Miezi mwili iliyopita, rais wa Sudan Omar al Bashir alizuru Juba na kukutana na mwenyeji wake rais Salva Kirr na kuzungumzia maswala ya usalama katika mipaka ya mataifa hayo mawili katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini na pia kuafikiana kuhusu maswala ya usafirishaji wa mafuta.

Maelfu ya waakazi wa majimbo hayo ya Blue Nile na Kordofan Kusini wameendelea kukimbia makwao kutokana na uvamizi kutoka kwa waasi wa SPM-N.

Sudan imeichukulia hatua Sudan Kusini ambayo inaadhimisha miaka miwili mwezi ujao tangu ilipojitenga na Sudan na kuwa taifa huru.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.