Pata taarifa kuu
Sudani

Waziri wa mambo ya nje wa Sudani azuru Juba

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali Ahmed Karti anazuru Sudan Kusini Ijumaa hii, miongoni mwa malengo ya ziara hiyo ni kuwasilisha barua ya Rais Omar Hassan al-Bashir kwa rais wa Sudan Kusini Salva Kiir juu ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili, shirika la habari la SUNA limeripoti. 

Waziri wa mambo ya nje wa Sudani Ali Ahmed Karti
Waziri wa mambo ya nje wa Sudani Ali Ahmed Karti iislamtimes.org
Matangazo ya kibiashara

Waziri Karti ameambatana na mkuu wa Usalama wa Taifa wa Sudan Mohamed Atta katika ziara hiyo ambayo ni ya kwanza tangu serikali ya Khartoum kuishutumu Juba kwa kuwaunga mkono waasi walioendesha shambulizi majuma matatu yaliyopita.

Mataifa hayo mawili kwa pamoja walikubaliana kuanza uzalishaji wa mafuta ambao ulisitishwa tangu mwaka 2011.

Wanadiplomasia wanaamini pande hizo mbili zilizozozana kwa muda mrefu wataendelea kuimarisha uhusiano wao uliochangiwa na maswala ya mipaka na biashara ya mafuta.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.