Pata taarifa kuu
KENYA

Oparesheni yafanyika kuwasaka waliotekeleza mauaji ya watu 10 mjini Garrisa

Polisi mjini Garissa nchini Kenya wanafanya msako mkubwa kuwasaka watu waliotekeleza shambulizi ndani ya Mkahawa mmoja mjini humo na kusababisha vifo vya watu kumi.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema kuwa kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa bastola aina ya AK47 waliwashambulia watu wao wakati walipokuwa wanatazama runinga siku ya  Alhamsihi usiku.

Kamanda wa polisi katika mkoa wa Kaskazini Mashariki Charlton Mureithi amesema ni mapema kufahamu ni akina nani waliotekeleza shambulizi hilo na kwa sababu gani.

Mji wa Garrisa unapakana na Somalia na zaidi ya wakimbizi 500,000 raia wa Somalia wanaishi katika mji huo ambao una hofu ya kuwahifadhi wanamgambo wa Al-Shabab kutoka nchini Somalia.

Wanagambo hao wamekuwa wakitishia kutekeleza mashambulizi dhidi ya wakenya kutokana na jeshi lao kuwa nchini humo kuanzia mwaka 2011 kupambana nao.

Wakati hayo yakijiri watu 63 wamepoteza maisha na wengine  zaidi ya 30,000 kukimbia makwao kutokana na mafuriko makubwa yanayoendelea kushuhudiwa nchini Kenya kwa sababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali katika taifa hilo.

Naibu wa rais William Ruto ametangaza idadi hiyo jijini Nairobi na kusema kuwa serikali imetoa vyakula na mahema kuwasaidia walioathirika na mafuriko hayo mabaya kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika siku za hivi karibuni.

Tayari serikali jijini Nairobi imetuma tani 5 ya vyakula mbalimbali katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuraiko hayo hasa majimbo ya Kaskazini, Pwani na Magharibi mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.