Pata taarifa kuu
KENYA

Mafuriko nchini Kenya yasababisha vifo vya watu 63

Watu 63 wamepoteza maisha na wengine  zaidi ya 30,000 kukimbia makwao kutokana na mafuriko makubwa yanayoendelea kushuhudiwa nchini Kenya kwa sababu ya mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali katika taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Naibu wa rais William Ruto ametangaza idadi hiyo jijini Nairobi na kusema kuwa serikali imetoa vyakula na mahema kuwasaidia walioathirika na mafuriko hayo mabaya kuwahi kushuhudiwa nchini humo katika siku za hivi karibuni.

Aidha, Ruto ameongeza kuwa serikali imeweka mikakati kabambe ya miaka 20 kukabiliana na mafuriko mengine kama hayo ikiwa yatatokea tena.

Tayari serikali jijini Nairobi imetuma tani 5 ya vyakula mbalimbali katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuraiko hayo hasa majimbo ya Kaskazini, Pwani na Magharibi mwa nchi hiyo.

Serikali jijini Nairobi imeagiza wanajeshi kuwasaidia watu walioathiriwa na mafuruko hayo na kuwahamisha katika maeneo salama ili kuepuka hasara kubwa ikiwemo kupoteza maisha.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo inasema kuwa huenda mvua hiyo ikaendelea kunoyesha hadi mwisho wa mwezi wa Aprili na huenda mafuriko zaidi yakatokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.