Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Makabiliano kati ya waasi wa Seleka na raia wasababisha zaidi ya vifo vya watu 10

Watu 12 waliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati wa makabiliano ya waasi wa Seleka na raia jijini Bangui na viunga vyake baada ya kuipindua serikali mwezi uliopita.

Combattants de la Seleka devant le palais présidentiel à Bangui, le 25 mars 2013.
Combattants de la Seleka devant le palais présidentiel à Bangui, le 25 mars 2013. REUTERS/Alain Amontchi
Matangazo ya kibiashara

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo limesema kuwa makabiliano kati ya raia na kundi hilo yalianza baada ya waasi hao wa Seleka kuanza kusaka silaha miongoni mwa raia jijini humo.

Hata hivyo, shirika hilo linasema kuwa huenda watu waliouliwa ni wengi na ni zaidi ya   20, na walioshuhudia makabaliano hayo wanasema kuwa waliwaona waasi wa Seleka wakiwafwatulia risasi raia hao.

Kundi hilo la Seleka limeshindwa kuimarisha usalama jijini Bangui baada ya kuchuka uongozi nchini humo huku mashirika ya Kimataifa ya kutoa misaada yakisema kuwa raia nchini humo wanahitaji maji, chakula na makaazi mengine muhimu ili kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Mwishoni mwa juma lililopita baraza la mpito nchini humo lilimchagua kiongozi wa waasi ambaye aliongoza mapinduzi ya serikali mwezi uliopita Michel Djotodia, kuwa rais wa mpito.

Djotodia, ameahidi kuhakikisha zoezi la uchaguzi linafanyika ndani ya miezi kumi na nane ijayo huku awali akisema lingefanyika baada ya miaka 3 kupita.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.