Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Watoto watumiwa kwenye mapigano nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la kuhudumia watoto duniani la Umoja wa Mataifa UNICEF limebaini uwepo mkubwa wa matumizi ya watoto katika makundi ya wapiganaji nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Shirika hilo limesema watoto hao wavulana kwa wasichana zaidi ya 2,000 wamekuwa wakihusishwa katika shughuli za wapiganaji hao.

REUTERS/Alain Amontchi
Matangazo ya kibiashara

Watoto hao wamekuwa wakitumiwa na pande zote zinazohusika na migogoro ya kisiasa kama wapelelezi, wajumbe na wakati mwingine kushirikishwa katika mapigano.

Akiwa mjini Ganava Msemaji wa UNICEF Marixie Mercado amewaambia waandishi wa habari kuwa katika kipindi cha miezi minne iliyopita usalama wa watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati hali umekuwa ni wa kusuasua.

Aidha Mercado ametoa wito kwa uongozi mpya wa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati wa kundi la waasi wa Seleka wanaoongozwa na Michel Djotodia kuhakikisha watoto wanaondolewa kwenye makundi ya wapiganaji.

Tangu mwaka 2007, UNICEF imewaokoa zaidi ya watoto 1,000 kutoka makundi ya wapiganaji katika maeneo yenye mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.