Pata taarifa kuu
SUDANI-UGANDA

Serikali ya Khartoum yashusha lawama kwa majeshi ya Uganda kuwaunga mkono waasi

Jeshi la Uganda la UPDF kwa mara nyingine tena limekanusha shutuma kutoka Serikali ya Khartoum kuwa linawaunga Mkono Waasi wanaopambana na serikali ya rais Omar al Bashir wenye kuwa na lengo la kuiangusha serikali. Jeshi hilo la UPDF limesema habari hizo hazina ukweli ndani yake badala yake limesema serikali ya Kharthoum imekuwa ikitowa ushirikiano kwa kundi la waasi wa LRA la Joseph Konny na kwamba wanaushahidi wa kutosha kuhusu hilo.

msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye
msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye
Matangazo ya kibiashara

Hii si mara ya kwanza serikali ya Kharthoum inaituhumu Uganda kuwapa msaada wa kijeshi waasi wanaopambana na serikali ya Sudani ili kuuangusha utawala wa  rais Omar Hassan al Bashir.

Msemaji wa jeshi la UPDF luteni kanali Felix Kulayigye amesema wanashtushwa na kauli za serikali ya Khartoum kuwaita kuwa maaduwi, na kwamba hawana sababu ya kuunga mkono waasi wa Sudani, kwa sasa ameendelea kusema kwamba kauli kama hizo za kichochezi wanazitupilia mbali.

Felix Kulayigye amesema, hakuna jipya katika hili kwani serikali ya khartouh imekuwa ikitowa kauli kama hizo, kwa sasa waganda wamezoea kusikia kauli kama hizo, lakini ukweli ni kwamba serikali ya kharthoum imewahi kumficha Joseph Konny na kutowa mafunzo kwa jeshi lake, kwa hiyo amesema hakuna jipya muhimu ni kwamba wananchi wa Uganda wanauaminifu na jeshi lao na kwamba linauwezo wa kuwalinda.

Makundi ya waasi yanaendelea kuhatarisha uslama katika eneo kubwa la ukanda wa afrika mashariki na kati, huku juhudi za kuyamaliza makundi hayo zikifanyika bila ufanisi wowote.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kuwa, Choko choko hizi baina ya serikali ya Karthoum na Kampala huenda zikazua mgogoro baadae iwapo viongozi wa pande mbili hawatolitafutia ufumbuzi wa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.