Pata taarifa kuu
SUDAN

Rais wa Sudan Omar Al Bashir atangaza kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa wanaoshikiliwa kwenye magereza

Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir ametangaza mpango wa kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa hatua ambayo ataamini itamaliza hofu iliyojengeka miongoni mwa Viongozi wa Kisiasa.

Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir ambaye ametangaza mpango wa kuwaachia wafungwa wa kisiasa
Rais wa Sudan Omar Hassan Al Bashir ambaye ametangaza mpango wa kuwaachia wafungwa wa kisiasa
Matangazo ya kibiashara

Rais Al Bashir ametangaza hatua ya kuwaachia wafungwa wa kisiasa wakati akihutubia Bunge na kusema wakati umefika sasa kwao kusaka mbinu mbadala za kushughulikia masuala ya kisiasa.

Al bashir akihutubia wabunge ambao wanaanza mhula mpya wa vikao vya Bunge ametaka wanasiasa kufahamu hiki ni kipindi cha mabadiliko ya kisiasa na hivyo serikali ya Khartoum itafanya kila linalowezekana kutimiza lengo lao.

Kiongozi huyo wa Sudan ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC amesema wakati umefika sasa kwa serikali yake kutumia njia ya majadiliano kushughulikia matatizo ya kisiasa.

Al Bashir amesema wataendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na wanasiasa pamoja na makundi ya kijamii yenye nguvu katika nchi hiyo lengo likiwa ni kupata ustawi mwema wa taifa la Sudan.

Uamuzi wa Rais Al Bashir umepokelewa kwa mikono miwili na Viongozi wa Kisiasa ambao wamesema utasaidia kwa kiasi kikubwa kuanza kwa mazungumzo ili kumaliza malumbano ya kisiasa.

Kiongozi wa Muungano wa Vyama Vya Upinzani zaidi ya 20 nchini Sudan Farouk Abu Issa amesema hatua ya Rais Al Bashir ni mwanzo mwema wa kukomaa kwa demokrasia katika nchi hiyo.

Issa amesema Kundi la Waasi la SPLM-N linalopambana na Majeshi ya Serikali kwa kipindi cha miaka miwili katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile walikuwa wanataka kuachiwa kwa wafungwa wao.

Kiongozi huyo wa Upinzani amesema kuna wafungwa 118 wakiwemo waasi wa SPLM-N ambao wanashikiliwa katika Majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile kama wakiachiwa itakuwa hatua nzuri.

Mwenyekiti wa Kundi la Waasi la SPML-N Malik Agar amesema wamelisikia tangazo la Rais Al Bashir lakini hawana uhakika kama wapiganaji wao watakuwa ni miongoni mwa wale watakaowekwa kwenye kundi la Wafungwa wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.