Pata taarifa kuu
DRC

Wanaharakati wataka majeshi ya serikali ya DRC yaondolewe mjini Kitchanga

Wanaharakati na Wasimamizi wa mashirika ya kiraia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameiomba serikali kuwaondoa wanajeshi wake katika mji wa Kitchanga mtaani Masisi siku chache baada ya kuwepo mapigano makali kati ya jeshi la serikali FARDC na wapiganaji wa Mai Mai wa APCLS.

AFP PHOTO/PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wataka majeshi ya serikali ya DRC yaondolewe mjini Kitchanga
Wanaharakati na Wasimamizi wa mashirika ya kiraia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wameiomba serikali kuwaondoa wanajeshi wake katika mji wa Kitchanga mtaani Masisi siku chache baada ya kuwepo mapigano makali kati ya jeshi la serikali FARDC na wapiganaji wa Mai Mai wa APCLS.

Baadhi ya Wanaharakati hususani kutoka kabila la Hunde wamelishutumu jeshi hilo kuwa lina ushirikiano wa karibu na waliokuwa waasi wa CNDP.

Msemaji wa majeshi ya Umoja wa mataifa Felix Basse amesema Jeshi la Umoja wa Mataifa linazidi kupiga doria katika mji huo na vikosi vyao vilifanikiwa kuwazuia wapiganaji wa Mai Mai kuzidi kusonga mbele.

Katika hatua nyingine aliyekuwa msemaji wa kundi la waasi wa M23 linalokabiliana na serikali ya DRC Bertrand Bissimwa ameteuliwa kuwa mkuu wa kisiasa wa kundi hilo siku chache tu baada ya kutimuliwa kwa Bishop Jean-Marie Runiga aliyekuwa kiongozi wa kisiasa wa kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.