Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Dhamana ya polisi wanane wa Afrika Kusini yacheleweshwa

Dhamana ya Polisi wanane nchini Afrika Kusini,wanaotuhumiwa kwa mauaji ya dereva taxi raia wa Msumbiji ambaye aliburuzwa kuelekea kituo cha polisi nyuma ya gari la polisi na kufariki dunia, imeahirishwa kusikiliza leo Jumatatu. 

Maafisa wakimwadhibu mtuhumiwa kabla ya kifo chake
Maafisa wakimwadhibu mtuhumiwa kabla ya kifo chake feeds.cbsnews
Matangazo ya kibiashara

Maafisa hao wanane walitarajiwa kujitokeza mahakamani kuomba dhamana baada ya kufunguliwa mashataka ya mauaji ya Mido Macia aliyekuwa na umri wa miaka 27.

Hata hivyo kesi hiyo imecheleweshwa bila washitakiwa kutokea mahakamani huku kukiwa na hofu ya wao kupigwa picha na kutambuliwa.

Hakimu Samuel Makamu ameridhia kesi hiyo kuendelea siku ya Ijumaa mara baada ya mashahidi wa serikali watakapo thibitisha utambulisho wa watuhumiwa.

Jumanne iliyopita dereva tax huyo raia wa Msumbiji alionekana akifanyiwa unyama kwa kufungwa nyuma ya gari la polisi kisha kuburuzwa hadi kituo cha polisi cha Daveyton, mashariki mwa Johannesburg, ambapo saa mbili baadaye alikutwa akiwa amekufa ndani ya chumba cha mahabusu ambapo uchunguzi ulibaini ya kwamba alifariki kutokana na majeraha ya kichwa na damu kuvuja kwa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.