Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Waasi wa Seleka waunga mkono Tingaye kuwa waziri mkuu nchini Jamhuri Afrika ya Kati

Muungano wa waasi wa Seleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamesema kuwa wanaunga mkono kiongozi wa upinzani Nicolas Tiangaye kuwa waziri mkuu katika mchakato uliotangulia makubaliano ya amani yaliyofikiwa juma lililopita. 

Rais wa C.A.R François Bozizé-kulia akiwa na mwakilishi wa  Seleka Michel Djotodia nchini Gabon
Rais wa C.A.R François Bozizé-kulia akiwa na mwakilishi wa Seleka Michel Djotodia nchini Gabon AFP PHOTO / STEVE JORDAN
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na AFP mjini Brazzaville baada ya mazungumzo na rais wa Congo Denis Sassou Nguesso ambaye anaongoza tume inayofuatilia makubaliano hayo, kiongozi wa kundi hilo Michel Djotodia amesema kuwa hawana pingamizi kuhusu bwana Tiangaye kuwa waziri mkuu ajaye.
 

Djotodia na wajumbe kadhaa wa waasi hao waliongozwa katika mkutano na Tiangaye , mwanasheria ambaye juma lililopita alichaguliwa na upinzani kuwa mkuu wa serikali katika taifa hilo lililokumbwa na machafuko.
 

Makubaliano ya amani yalitiwa saini baina ya waasi, chama tawala na chama cha upinzani Ijumaa iliyopita mjini Libreville nchini Gabon kwa lengo la kumaliza uasi ulioanza tarehe kumi mwezi Disemba mwaka jana Kaskazini mwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kushuhudia waasi wakipiga hatua kuelekea mji mkuu wa Bangui.
 

Jumuiya ya Kimataifa imekuwa ikishiniza serikali ya rais Bozize na viongozi wa waasi kupata suluhu la kudumu ili kurejesha amani nchini humo na kuzuia maelfu ya watu kukimbia makwao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.