Pata taarifa kuu
Mali

Wanajeshi 12 wa Serikali ya Mali wadaiwa kutekwa na Waasi wa nchi hiyo

Waasi wa nchini Mali wameteka wanajeshi wa Serikali 12 sambamba na Magari yao na vifaa vyao vya kazi, Taarifa zimeeleza.

Waasi wa Ansar Dine wakiwa  mjini Azawad kaskazini mwa Mali
Waasi wa Ansar Dine wakiwa mjini Azawad kaskazini mwa Mali AFP/YouTube
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea jana wakati wa Doria nje ya mji wa Kona karibu na mji wa Mopti, wakati kukiwa na hali ya wasiwasi kuwa Waasi wanaoshikilia eneo la kaskazini mwa Mali , wanaendelea kusogelea karibu maeneo yanayodhibitiwa na Serikali ya nchi hiyo.
 

Mapema hapo jana Wanajeshi wa Serikali walipambana na kundi la Waasi wenye mashirikiano na kundi la wanamgambo wa Al Qaeda, Ansar Dine.
 

Makundi makubwa yakiwa na magari wameripotiwa kukaribia Mji wa Mopti ambapo majeshi ya Serikali yamekita kambi huku Msemaji wa Waasi wa Ansar Dine amekanusha taarifa ya kuwa wamekuwa wakikaribia katika maeneo yanayodhibitiwa na Vikosi vya Serikali.
 

Serikali ya Mali ilipoteza udhibiti wa eneo la kaskazini mwa Mali baada ya Waasi kutumia mwanya wa Mapinduzi ya kijeshi kumuondoa Rais aliyechaguliwa kidemokrasia.
 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha hatua za kijeshi kuchukuliwa , hata hivyo limetaka kwanza kufanyika mchakato wa makubaliano ya kisiasa kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.