Pata taarifa kuu
MISRI

Rasimu ya katiba mpya yapitishwa rasmi nchini Misri

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Misri imethibitisha rasmi matokeo ya kura ya maoni na kuipa ushindi kura ya ndiyo na hivyo kupitishwa kwa katiba mpya ya nchi hiyo baada ya asilimia sitini na nne ya wapiga kura kuunga mkono rasimu.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Rais Mohamed Morsi na vyama ambavyo vinamuunga mkono kikiwemo chama tawala cha Muslim Brotherhood ndivyo vimeibuka na ushindi kwenye kura hiyo ya maoni huku upinzani ukindelea kulalama kuwa kumekuwa na hila katika mchakato wa kupitishwa kwa katiba hiyo.

Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil amesema hakuna upande ambao umeshindwa kwenye kura ya maoni kwa kuwa katiba mpya itakuwa ya wananchi wote kipindi hiki ambacho upinzani unaendelea kupinga.

Kwa upande wake msemaji wa wapinzani wa muungano wa National Salvation Front Khaled Daoud amesema tayari wameshawasilisha madai yao katika ofisi ya Mwendesha Mashtaka kupinga udanganyifu uliofanywa ili kupitisha rasimu ya katiba.

Muungano huo umeapa kuendeleza harakati zake kuhakikisha Wamisri wanapata katiba watakayoichagua wao wenyewe hali ambayo inazua hofu ya kuibuka kwa mzozo zaidi na kuendeleza wimbi machafuko yaliyodumu kwa takribani mwezi mmoja tangu Rais Mursi ajiongezee madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.