Pata taarifa kuu
MISRI

Maelfu ya waandamanaji wafurika jijini Cairo kabla ya kuanza kupiga kura

Maelfu ya waandamanaji kutoka upinzani na wafuasi wa rais Mohammed Morsi Ijumaa wamekusanyika jijini Cairo Misri kuipigia debe kura ya maoni kuhusu katiba mpya huku upinzani ukiwashawishi raia nchini humo kuipinga wakati wafuasi wa rais Morsi wakiwarai wananchi nchini humo kupiga kura ya ndio siku ya Jumamosi.

Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili limeigawa taifa hilo ambalo limekuwa likishuhudia maandamano makubwa katika siku za hivi karibuni na kusababisha watu saba kupoteza maisha huku mamia wakijeruhiwa.

Hata hivyo, wapiga kura katika miji mikubwa ya Cairo na Alexandria watapiga kura zao tarehe 22 kutokana na kutowepo na majaji wa kutosha kusimamia  zoezi hilo.

Upinzani nchini Misri unasisitiza kuwa utapinga rasimu ya katiba mpya ,huku wachambuzi wa siasa nchini humo wakisema kuwa huenda wapinzani wakasusia zoezi hilo.

Jeshi nchini humo awali lilikuwa limetoa wito kwa rais Mohammed Morsi kufanya mazungumzo na viongozi wa upinzani kwa ajili ya umoja nchini humo na kujadili rasimu hiyo lakini kikao hicho hakikufanyika kutokana na kila upande kuendelea kushikilia upande wake.

Serikali inasema zoezi hili litaendelea kama ilivyopangwa na tayari imeweka mikakati kwa majaji wengine kusimamia shughuli hiyo siku ya Jumamosi.

Upinzani unasema katiba hiyo ni mbaya, inawabagua wanawake na kuminya uhuru wa kujieleza pamoja na Wakiristo na wanataka ifanyiwe marekebisho kabla ya kupigiwa kura.

Upinzani umekuwa ukiandaa maandamano jijini Cairo na miji mingine nchini humo kupinga kufanyika kwa kura ya maoni na kusababisha mauaji ya watu saba na mamia wengine kujeruhiwa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.